Top-ads

By | 1:30 PM

MBUNGE SUMARI AFARIKI DUNIA

 

      Jeremiah Sumari.
Habari zilizotufikia asubuhi hii zinasema kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jeremiah Sumari amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Habari zinasema kuwa mbunge huyo aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi alikuwa akisumbuliwa na uvimbe kwenye ubongo kwa muda mrefu.
Imeelezwa kwamba kuna kipindi hali yake ilikuwa mbaya ambapo alipelekwa kutibiwa nchini India.
Baada ya kupata matibabu, alirudishwa nchini ambapo amefariki saa 8 usiku wa kuamkia leo akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mtandao huu unatoa pole kwa wote waliofikwa na msiba huu!


MISA YA MAZISHI YA MAREHEMU REGIA MTEMA YAFANYIKA IFAKARA LEO

Misa Maalum ya Mazishi ya kumwombea aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Marehemu Regia Mtema ikiendelea Ifakara Morogoro leo mchana, muda mfupi kabla ya mazishi.

Naibu Spika, Job Ngugai (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Kiongozi wa Kambi ya Upinzania na Mbunge wa Hai, Mheshimiwa Freeman Mbowe pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mheshimiwa Zitto Kabwe wakifuatilia kwa makini Misa Maalum ya Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Marehemu Regia Mtema Ifakara leo.
Sehemu ya umati mkubwa wa waombolezaji wakifuatilia kwa ukaribu Misa Maalum ya Mazishi ya liyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Marehemu Regia Mtema Ifakara Morogoro leo. Picha kwa hisani ya HAKINGOWI.COM
Newer Post Home