PADRI AFUMANIWA LIVE NA MKE WA MTU AKIWA UCHI WA MNYAMA
KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya
padri wake,Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa
kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu.
Father Ngowi akiwa ameduwaa baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita
chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi Vijijini ambako Father
Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana
kwa jina la kijamii la Mama P.
Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!
Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri
huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya
madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi
huyo wa Mungu.
“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu
wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini
akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.
Father Ngowi akijaribu kuomba samahani baada ya kufumaniwa.
Chanzo kikaendelea kudai kwamba baada ya kuona mkewe amejikita kwa
mtumishi wa Mungu, mumewe alinyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.
Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya ndugu wa mume kumfuatilia mpaka anaingia
kwa Father Ngowi, wakaona ni bora watafute mpigapicha ili kupata picha
za tukio ambazo zitakuwa ushahidi siku za mbele.
“Walipompata wakazama ndani, sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta mwanamke huyo na mtumishi wa Mungu wapo kitandani.”
Father Ngowi na Mama P wakivaa nguo zao kwa aibu baada ya kufumaniwa.
Habari zinadai kwamba kufuatia tukio hilo, tayari Kanisa Katoliki
limemweka kitimoto padri huyo ambaye alikuwa akihudumu katika Parokia ya
Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishwa na kupelekwa Parokia ya
Makomu, Marangu ambako inadaiwa ameshushwa cheo.
Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo, Father Ngowi alikana kukutwa na mke
wa mtu chumbani kwake lakini alipobanwa sana na mabosi wa Jimbo Kuu la
Kanisa Katoliki Moshi, alikiri na kudai ibilisi alimpitia na kuomba
kanisa limsamehe na kutompa adhabu kali ambayo itamuathiri kisaikolojia.
Hili ni tukio kubwa na la aina yake kuwahi kulikumba Kanisa Katoliki
nchini kwa padri wake kudaiwa kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake!
Father Ngowi na Mama P wakiwa na nyuso za aibu baada ya tukio hilo.
Kuna madai kwamba mwaka jana (2012), Father Ngowi, mbele ya waumini wake
alisoma barua yenye kukana shutuma zote zilizoelekezwa kwake kwamba
amekuwa na ukaribu wenye maswali mengi na wake za watu.
Taarifa zilidai kuwa padri huyo aliweka wazi akisema si kweli kwamba
amekuwa na ukaribu unaotajwa, akawataka waumini wake wapuuze tuhuma hizo
alizosema zina mwelekeo wa kuchafua sifa yake na taswira ya Kanisa
Katoliki kwa jumla.
Hayo ni madai ya vyanzo vyetu ambavyo viliambatanisha na picha
mbalimbali za tukio hilo lenye kushtua waumini sambamba na namba za simu
za padri huyo kwa ajili ya mawasiliano ili kujiridhisha.
Father Ngowi akipatiwa suruali yake.