Zuku
ilizinduliwa rasmi jana usiku katika sherehe ya kufana iliyofanyika
kwenye ukumbi wa Golden Tulip. Sherehe hii ilihudhuriwa na wajumbe,
waingizaji, wajasiriamali na watu mbalimbali walioshuhudia uzinduzi wa
Zuku TV.
Mwenyekiti
wa Wananchi Group, mheshimiwa Ali Mufuruki aliongelea mfumo mzima wa
kiufundi wa runinga, ikifuatiwa na maonesho ya fataki na pia burudani
toka kwa wasanii mbalimbali kuwadhihirisha wageni wote.
"Tunayo
furaha kuzindua TV ya Zuku hapa Tanzania," Alisema Richard Bell, Afisa
mkuu mtendaji wa Wananchi Group. "Ni hatua kubwa kwetu na…

Zuku
ilizinduliwa rasmi jana usiku katika sherehe ya kufana iliyofanyika
kwenye ukumbi wa Golden Tulip. Sherehe hii ilihudhuriwa na wajumbe,
waingizaji, wajasiriamali na watu mbalimbali walioshuhudia uzinduzi wa
Zuku TV.
Mwenyekiti
wa Wananchi Group, mheshimiwa Ali Mufuruki aliongelea mfumo mzima wa
kiufundi wa runinga, ikifuatiwa na maonesho ya fataki na pia burudani
toka kwa wasanii mbalimbali kuwadhihirisha wageni wote.
"Tunayo
furaha kuzindua TV ya Zuku hapa Tanzania," Alisema Richard Bell, Afisa
mkuu mtendaji wa Wananchi Group. "Ni hatua kubwa kwetu na tunafarijika
kuweza kutoa burudani bora majumbani kwa watu wote.
Televisheni
ya Zuku inatoa uchaguzi mpana wa stesheni za burudani ikiwa ni pamoja
na Habari, Michezo na Sinema, majarida na muziki. Hivi vinajumuisha
chaneli za nje kama vile BBC, MTV Base, Sentanta Sports, MGM movies na
zinginezo nyingi. Pia Msambazaji hutoa ofa kabambe za stesheni kama vile
Zuku Afrika ambayo huonesha bara la Afrika, Zuku Maishaambayo huonesha
makala mbalimbali, Zuku Michezo pamoja na chaneli lukuki za sinema.
Huduma hii ya Zuku hupatikana kupitia satelaiti Tanzania nzima.

Mkurugenzi wa TCRA,Profesa
John Mkoma mbele ya wageni waalikwa mbalimbali kabla ya kuzindua
kampuni ya Wananchi Satelite jana katika hafla iliyofanyika jana kwenye
hoteli ya Golden Tulip kulia ni Richard Bell Afisa
Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group na kulia ni Mwenyekiti wa
makampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufuruki
Mwenyekiti wa makampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufuruki akizungumza katika uzinduzi huo na kumkaribisha Mkurugenzi wa TCRA Profesa John Mkoma.

Richard Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group akimkaribisha Mwenyekitiwa Makampuni ya Wananchi Group Ali Mufuruki.
Kundi la TMK wanaume Family likitumbuiza katika uzinduzi huo jana.
Bendi ya Tanzanite ikiongozwa na mwanamzuiki nguli John Mhina ilitoa burudani ya kutosha katika uzinduzi huo jana.
Wadau hawa nao walikuwepo ndani ya nyumba kama unavyowaona wengi wanaipenda ZUKU TV.
Waimbaji
wa muziki wa injili pamoja na waigizaji wa filamu hawakukosa uzinduzi
huop kutoka kulia ni Mwigizaji Natasha, Monalisa , Mwimbaji Alice na
mumewe ambaye pia ni mwimbaji Bw. Robert David wakipozi kwa picha.
Richard
Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group katikati na
Mwenyekiti wa makampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufuruki kulia wakimsikiliza Meneja mkuu wa Wananchi Satelite Bw Mohamed Jeneby akiwaelezea jambo.
Richard
Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group kulia i na
Mwenyekiti wa makampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufurukiwakijadili jambo katika uzinduzi huo.
Wadau kutoka ZUKU TV wakipozi kwa picha jana katika uzinduzi huo.
Mamaa Shamimu Mwasha a.k.a. ZEZE wa http://8020fashions.blogspot.com/akitafuta taswira katika uzinduzi huo, kuminya jicho ni lazima kama unataka taswira iliyotukuka.
Kutoka kulia ni wadau ZIZZOU wa ZIZZOU Fashion, Suzy wa Clouds na mdau Godliver wa Prime Time wakipozi kwa picha.
chnzo na http://fullshangwe.blogspot.com/
Zuku
ilizinduliwa rasmi jana usiku katika sherehe ya kufana iliyofanyika
kwenye ukumbi wa Golden Tulip. Sherehe hii ilihudhuriwa na wajumbe,
waingizaji, wajasiriamali na watu mbalimbali walioshuhudia uzinduzi wa
Zuku TV.
Mwenyekiti
wa Wananchi Group, mheshimiwa Ali Mufuruki aliongelea mfumo mzima wa
kiufundi wa runinga, ikifuatiwa na maonesho ya fataki na pia burudani
toka kwa wasanii mbalimbali kuwadhihirisha wageni wote.
"Tunayo
furaha kuzindua TV ya Zuku hapa Tanzania," Alisema Richard Bell, Afisa
mkuu mtendaji wa Wananchi Group. "Ni hatua kubwa kwetu na tunafarijika
kuweza kutoa burudani bora majumbani kwa watu wote.
Televisheni
ya Zuku inatoa uchaguzi mpana wa stesheni za burudani ikiwa ni pamoja
na Habari, Michezo na Sinema, majarida na muziki. Hivi vinajumuisha
chaneli za nje kama vile BBC, MTV Base, Sentanta Sports, MGM movies na
zinginezo nyingi. Pia Msambazaji hutoa ofa kabambe za stesheni kama vile
Zuku Afrika ambayo huonesha bara la Afrika, Zuku Maishaambayo huonesha
makala mbalimbali, Zuku Michezo pamoja na chaneli lukuki za sinema.
Huduma hii ya Zuku hupatikana kupitia satelaiti Tanzania nzima.

Richard Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group akimkaribisha Mwenyekitiwa Makampuni ya Wananchi Group Ali Mufuruki.
Bendi ya Tanzanite ikiongozwa na mwanamzuiki nguli John Mhina ilitoa burudani ya kutosha katika uzinduzi huo jana.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika uzinduzi huo.