BOMU LALIPUKA MOI AVENUE NAIROBI KENYA
Massive
blast rocks building housing several clothing stalls on Moi Avenue near
the Mount Kenya University. Scores injured: deaths unclear
![]() |
Add caption |
Kumetokea mlipuko katika mji mkuu nchini Kenya,Nairobi.
Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada ya saa
saba mchana saa za Afrika Mashariki katika barabara ya Moi kwenye jumba
moja la kibiashara lililo pia sehemu ya chuo kimoja kikuu cha kibinafsi
nchini humo.Haijafahamika chanzo cha mlipuko huo. Makundi ya waokoaji yanaendelea na shughuli ya uokoaji.
Kumekuwa na milipuko kadhaa nchini Kenya tangu taifa hilo lilipotuma majeshi yake nchini Somalia kukabiliana na kundi la kigaidi la al-shabab.
Kundi hilo limeshutumiwa katika siku za hivi karibuni kwa mashambulio kadhaa nchini humo..