Top-ads

By | 1:20 AM

MPANGO MPYA WA ULIMWENGU

Naamini watu wengi wameshasikia juu ya kile kinachojulikana kama Mpango Mpya wa Ulimwengu (New World Order). Hata hivyo, wapo pia wengine wengi ambao hawana habari juu ya kile kinachoendelea kuhusiana na mpango huu.
Mpango Mpya wa Ulimwengu ni mpango wenye nia ya kuusuka ulimwengu upya ili uweze kuwa tofauti na ulivyo sasa; ili uweze kuendana na malengo ya hao wanaoutaka. Mpango huu ni mkakati kabambe unaosimamiwa na watu wenye nguvu duniani, yaani wenye nguvu za kiuchumi, kisiasa, na hata kiroho.
Malengo ya mpango huu ni mengi. Kati yake ni haya yafuatayo:
  • Kuwa na serikali moja inayotawala dunia yote.
  • Kuwa na mfumo mmoja wa fedha duniani kote.
  • Kuwa na uchumi mmoja duniani kote.
  • Kuwa na dini moja duniani kote.
  • Kuwa na jeshi moja linalosimamia ‘amani’ duniani kote.
  • Kuwa na dunia yenye watu wasiozidi bilioni moja tu.
  • Kuwa na makundi mawili tu ya watu, yaani watawala na watumishi.
  • Utawala utakuwa ni wa kurithi; si wa kuchaguliwa. Yaani unakuwa mikononi mwa kundi lilelile.
  • Kutokuwapo kwa mipaka iliyopo leo ambayo inatenganisha mataifa.
  • Kuwa na udhibiti kikamilifu juu ya kila mwanadamu ambaye atakuwapo duniani wakati huo.
Katika utawala wa dunia chini ya mpango huu, maisha ya watu yatakuwa yanasimamiwa na serikali itakayokuwapo. Wale watakaokuwa watii kwa utawala, wataweza kupata mahitaji yote, kama vile chakula, maji, matibabu, n.k.
Wale ambao watakuwa wakaidi, watanyimwa kila huduma hadi wafe kwa njaa na magonjwa. Pia, kama ilivyo kwa tawala zote za kidikteta, watu watakuwa wakiishi kwa kuogopana wenyewe kwa wenyewe. Propaganda zitafanya kazi yake kuwajaza watu mawazo kwamba, kila aliye kinyume na serikali ni adui wa umma. Kwa hiyo, yeyote atakayemwona mtu wa namna hiyo atatakiwa amripoti kwenye vyombo vya usalama, au hata kumwua.
Naamini wengi tunakumbuka jinsi tawala za kijamaa na kikomusti zilivyokuwa – yaani tawala kama vile za Urusi, China, Korea Kaskazini, Ethiopia ya Mengistu, nk, na hata mataifa mengine ya kidikteta kama vile Irani. Mtu yeyote anayekuwa na mawazo tofauti na ya watawala; au anayehoji jambo lolote, anaitwa kibaraka wa mabeberu, mshirika wa maadui, msaliti wa umma, n.k. Kila mtu anakuwa anamwogopa mwenzake, maana hujui nani atakayeripoti kile utakachokisema. Ni maisha yaliyojaa hofu, woga na mateso mengi.
Je, viongozi wakubwa wa dunia wanasema nini juu ya jambo hili? Angalia mifano michache ifuatayo:
Henry Kissinger
Huyu alikuwa ni kiongozi mkubwa wa Marekani. Alikuwa ni Katibu Mkuu wa Nchi (Secretary of State). Yeye alisema:
Today America would be outraged if UN troops entered Los Angeles to restore order. Tomorrow they will be grateful. When presented with this scenario, individual rights will be willingly relinquished for the guarantee of their well-being granted to them by the World Government.
Yaani:
Leo Amerika itakasirika sana endapo majeshi ya Umoja wa Mataifa yataingia Los Angeles ili kurejesha amani. Kesho watafurahia jambo hilo. Itakapofikia hapo, itabidi watu wakubali kupoteza haki zao binafsi ili waweze kuwa na uhakika wa hali bora itakayotolewa na Serikali ya Kidunia.
David Rockefeller
Huyu ni mwanafamilia katika familia ya Rockfeller, ambao ni matajiri wakubwa sana Marekani. Yeye alisema:
We are grateful to the Washington Post, The New York Times, Time Magazine and their great publications whose directors have attended our meetings and respected their promises of discretion for almost forty years. It would have been impossible for us to develop our plan for the world if we had been subjected to the lights of publicity during those years. But, the world is now more sophisticated and prepared to march towards a world government. The supranational sovereignty of an intellectual elite and world bankers is surely preferable to the national auto-determination practiced in past centuries.
Yaani:
Tunawashukuru Washington Post, The New York Times, Time Magazine pamoja na machapisho yao bora, ambayo wakurugenzi wake wamehudhuria mikutano yetu na wameheshimu ahadi zao kwa karibu miaka arobaini. Isingewezekana kabisa kwa sisi kutengeneza mpango wetu kwa ajili ya dunia kama waandishi hawa wangeweka wazi mambo yetu kwa umma katika miaka hiyo yote. Lakini ulimwengu hivi sasa umeendelea sana na uko tayari kuelekea kwenye serikali ya dunia nzima. Serikali hiyo kuu ya wasomi wachache na wamiliki wa mabenki wa kidunia kwa hakika ndiyo inayofaa kuliko serikali za kitaifa ambazo zimekuwapo kwenye karne zilizopita.
George Bush Sr.
Huyu alikuwa ni rais wa Marekani. Ni baba yake na George Bush, aliyeendesha vita vya Iraki; ambaye naye alikuwa rais wa Marekani. Yeye alisema:
We have before us the opportunity to forge for ourselves and for future generations a new world order…. When we are successful, and we will be, we have a real chance at this new world order. An order in which a credible United Nations can use its peace keeping role to fulfill the promise and vision of the UN’s founders.
Yaani:
Mbele yetu tunayo fursa ya kujitengenezea mpango mpya wa dunia kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo ... Pale tutakapofanikiwa, na lazima tufanikiwe, tunayo nafasi ya kweli katika mpango huu mpya wa dunia. Ni mpango ambapo Umoja wa Mataifa unaoaminika unaweza kutumia jukumu lake la kulinda amani katika kutimiza ahadi na maono ya waasisi wa Umoja wa Mataifa.
Barack Hussein Obama
Huyu ni rais wa Marekani sasa. Yeye alisema :
All nations must come together to build a stronger global regime.
Yaani:
Mataifa yote ni lazima yaungane ili kujenga utawala wa kidunia wenye nguvu.
Walter Cronkite
Huyu alikuwa ni mtangazaji na mwandishi wa habari maarufu sana wa CBS News kule Marekani. Yeye alisema:
“It seems to many of us that if we are to avoid the eventual catastrophic world conflict we must strengthen the United Nations as a first step toward a world government patterned after our own government with a legislature, executive and judiciary, and police to enforce its international laws and keep the peace," he said. "To do that, of course, we Americans will have to yield up some of our sovereignty. That would be a bitter pill. It would take a lot of courage, a lot of faith in the new order. Pat Robertson has written in a book a few years ago that we should have a world government, but only when the Messiah arrives. He wrote, literally, any attempt to achieve world order before that time must be the work of the devil. Well, join me. I'm glad to sit here at the right hand of Satan.”
Yaani:
“Inaonekana kwa wengi wetu kuwa kama tunataka kuepuka migogoro mikubwa itakayotokea duniani ni lazima tuimarishe Umoja wa Mataifa kama hatua ya kwanza kuelekea kwenye serikali ya kidunia ambayo inafanana na serikali zetu zilizopo sasa, ikiwa na baraza la kutunga sheria, serikali na mahakama, polisi wa kusimamia sheria zake za kimataifa na kusimamia amani,” alisema. “Ili kufanya hayo, sisi Wamarekani inabidi tupoteze kiasi fulani cha mamlaka yetu. Hicho kitakuwa ni kidonge kichungu. Itahitaji ujasiri mkubwa, imani kubwa kwenye mpango mpya wa dunia. Pat Robertson ameandika kwenye kitabu miaka michache iliyopita kwamba tunatakiwa kuwa na serikali moja duniani, lakini ni pale tu atakapofika Masihi. Aliandika kuwa, juhudi zozote za kuwa na mpango mpya wa dunia kabla ya wakati huo ni lazima uwe ni kazi ya ibilisi. Basi, karibuni muungane nami. Nafurahia kukaa hapa kwenye mkono wa kulia wa Shetani.”
Jaque Chirac
Huyu aliwahi kuwa rais wa Ufaransa. Yeye alisema katika hotuba aliyotoa kule The Hague:
... that the UN’s Kyoto Protocol represented “the first component of an authentic global governance. For the first time, humanity is instituting a genuine instrument of global governance.”
Yaani:
... kwamba Mkataba wa UN wa Kyoto uliwakilisha “kipengele cha kwanza kinachohusu utawala wa kweli wa kidunia. Kwa mara ya kwanza, wanadamu wanaanzisha chombo cha kweli kinachohusu utawala wa kidunia.”
Strobe Talbott
Huyu alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Serikali (Deputy Secretary of State) wakati wa uongozi wa Bill Clinton. Yeye alisema:
In the next century (now), nations as we know it will be obsolete; all states will recognize a single global authority and realize national sovereignty wasn’t such a great deal after all.
Yaani:
Katika karne ijayo [yaani hii iliyopo], mataifa kama tunavyoyajua sasa, yatakuwa ni jambo lililopitwa na wakati; mataifa yote yatatambua mamlaka moja ya kilimwengu na kutambua kuwa utawala wa kitaifa unaotumika sasa, kumbe ulikuwa si chochote si lolote.
Mikhail Gorbachev
Huyu alikuwa rais wa Urusi, ambaye alichangia katika kuanguka kwa Umoja wa Urusi. Yeye alisema:
Further global progress is now possible only through a quest for universal consensus in the movement towards a new world order.
Yaani:
Maendeleo zaidi duniani hivi sasa yanawezekana tu endapo dunia yote itakubaliana kuelekea kwenye mpango mpya wa dunia.
Robert Kennedy
Huyu alikuwa ni mwanasiasa wa Marekani, ambaye alikuwa ni ndugu wa rais John F. Kennedy. Yeye alisema:
All of us will ultimately be judged on the effort we have contributed to building a New World Order.
Yaani:
Sisi sote tutahukumiwa kulingana na juhudi tulizochangia katika kujenga Mpango Mpya wa Ulimwengu.
Robert Mueller
Huyu alikuwa ni Mwanasheria Mkuu Msaidizi katika Umoja wa Mataifa. Yeye alisema:

We must move as quickly as possible to a one-world government, one-world religion, under a one-world leader.
Yaani:
Ni lazima tupige hatua haraka iwezekanavyo kufikia serikali moja ya duania nzima, dini moja ya dunia nzima, chini ya kiongozi mmoja wa dunia nzima.
Unaweza kusoma zaidi kuhusu nukuu hizo hapo juu kwa kubofya HAPA.
Haya rafiki yangu unayesoma makala haya. Sijui unajifunza nini kutokana na maneno haya ya wababe wa siasa na uchumi duniani? Kinachoonekana hapa ni kwamba, japo sisi wengine kunakucha, kunakuchwa, watu wako kwenye kazi usiku na mchana ambayo inalenga kutekeleza jambo hili. Na kazi hii imekuwa ikiendelea kwa miaka na miaka. Hivi sasa iko katika hatua za juu sana.
New World Order ndiyo hiyo inakuja. Sisi tumekaa tu tukidhani tunakula raha; vijana wako ‘bize’ tu kutembea na milegezo na kuhudhuria kwenye matamasha ya bongo fleva; akina dada nao wako ‘bize’ kujiremba na kujipodoa, wazee wako ‘bize’ na ufisadi maofisini ...nk.,  nk. Swali ni je, uko tayari kwa mambo ambayo yanaujia ulimwengu? Au nawe ni mmoja wa wale wanaosema, “Ah, wapi bwana! Hakuna kitu kama hicho!” Fungua macho yako! Mambo yanaenda kasi sana hivi sasa kuliko unavyoweza kufikiri.
Kwa kifupi, Mpango Mpya wa Ulimwengu ni suala linalosimamiwa na kundi linalojulikana kama Illuminati. Hii si mada ya makala haya, lakini Illuminati maana yake ni ‘the enlightened’, yaani wenye nuru au ufahamu. Hawa ni kundi kubwa la watu matajiri na wenye nguvu wanaodai kuwa wana maarifa au ufahamu maalumu, ambao ulimwengu uliobakia hatujui kinachoendelea.
Kimsingi sisi wengine wanatuita ni ‘useless eaters’, yaani watu wanaokula tu na kumaliza rasilimali za dunia lakini hawana faida yoyote. Ndiyo maana kuna haja kwao ya kupunguza watu hadi wasizidi bilioni moja.
Je, Biblia inasema chochote juu ya mambo haya? Jibu ni ndiyo.
Kitabu cha Daniel kiliandikwa karibia miaka 170 kabla ya Kristo, yaani miaka 2182 iliyopita. Danieli alionyeshwa na Mungu katika ndoto kile ambacho dunia ingepitia kwa habari ya tawala kuu nne. Katika ndoto hiyo alionyeshwa kuwa, utawala wa mwisho ungekuwa kama ifuatavyo:
Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi. (Danieli 7:7).
Ukiendelea kusoma, ufafanuzi unatolewa juu ya mnyama huyo.
Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande. (Danieli 7:23).
Huu kwa kifupi ni utawala wa kikatili, wa kidikteta. Ni utawala ambao ndio tumeusoma hapo juu, ambao umekuwa ukisukwa kwa miaka mingi chini kwa chini; na si ajabu, wengi wa watu waliopo sasa wakaweza kuushuhudia maishani mwao.
Nimekueleza kuwa lengo mojawapo muhimu la utawala huu katili ni kumdhibiti kila mwanadamu atakayekuwapo duniani wakati huo. Ili kufanya hivyo, nilikuambia kwenye makala yaliyopita kwamba watu watawekewa micro chip usoni au mkononi ili kuweza kuwafuatilia kila waliko. Hapa Bwana Yesu anasema:
Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. (Ufunuo 20:4).
Kwa wale watakaokuwa duniani, kama nilivyosema, itakuwa ni mateso na dhiki nyingi. Biblia inasema:
Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule. Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Mtu akiwa na sikio na asikie. (Ufunuo 13:1-9).
Tumeona kuwa kila atakayekataa kupigwa ile chapa ya utawala, atafuatiliwa, atatengwa, atateswa na hata kuuawa. Lakini kwa wale ambao watakuwa wamekubali kupokea chapa ya utawala huo, wataonekana kana kwamba wana raha, maana watapewa mahitaji yao ya kila siku na serikali. Lakini baada ya utawala huo kufikia mwisho, watakutana sasa na Mfalme wa wafalme, Yesu Kristo. Biblia inasema:
Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. (Ufunuo 14:9-10).
 Kazi ni kwako rafiki. Kila mara nimesema, shetani anakuja na Yesu naye anakuja. Sijui utakuwa upande gani? Sote sisi kila mmoja wetu anajua moyo wake ulivyo, hata kama mbele za wanadamu tutajaribu kujificha. Jambo moja la kufahamu ni kuwa, kila ambacho Bwana Yesu amekisema kwenye Biblia, ni lazima kitatokea. Lazima! Kuamini au kutoamini kwetu hakubadilishi chochote.
Bwana anasema: Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia. Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. (Mt. 24:34-35).
Kila kitu kiko wazi sana kwa yeyote aliye tayari kufungua macho yake na kuona. Lakini wakati huo utakapotimia kabisa, kila ambaye hayumo ndani ya safina (Yesu), atanaswa kama mtego unasavyo. Hakutakuwa na njia ya kujinasua hata kidogo. Huo ndio ukweli wenyewe. Ni juu yetu kurekebisha mambo yetu ya kiroho kungali na muda huu wa sasa. Mungu akubariki rafiki yangu. Njoo kwa Yesu upate salama ya maisha yako. Yesu ndiye mwenye mbingu na nchi. Ukimkataa, utakuja kwenda kwa nani?
 Wokovu wa Yesu ni bure kwa njia ya imani tu. Hakuna mwanadamu anayeweza kununua uzima wa milele kwa kujaribu kufanya matendo mema. Sijui iwapo tangu uanze juhudi za namna hiyo kama umefanikiwa. Wokovu ni kwa imani katika Yesu Kristo.
 Kwa wewe ambaye tayari unamwamini Yesu kama Mwokozi, endelea kung’ang’ania wokovu. Bwana anasema:
 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. (Ufunuo 3:10-11).
Songa mbele katika wokovu. Endelea kusimama imara katika imani!

Newer Post Older Post Home