ASANTE RAIS JAKAYA KIKWETE
Mwanamuziki wa Bongo Fleva maarufu kama Ray C siku ya leo amemtembelea Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu kipindi alipokuwa mgonjwa.Kwa upande wa mama mzazi wa Ray C amemshukuru sana Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Ray C kushoto,Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve( kushoto) na kulia ni Sarah Mtwere Dada yake Ray C.