SIKUWAHI PIGA PICHA ZA UCHI ILI NIWE MAARUFU....SHILOLE
MSANII ndani ya tasnia ya filamu na muziki, Zena Muhamed ‘Shilole’, ameamua kuongea kuwa
awali alipoigia kwenye tasnia ya filamu alikuwa anatafuta skendo lakini
hata hivyo hakuwahi kujiweka nusu uchi ili ajulikane kwani siku
ambayo atafanya hivyo ananaamini hata familia yake na hata mashabiki
wanaomkubali watamuona mtu wa ajabu sana"nilikuwa natafuta skendo kipindi cha nyuma lakini si kwa kukaa uchi" aliongea msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri mnoo na kundi lake lenye staili ya kanga moko.
Msanii
huyo alidai kuwa alikuwa na skendo nyingi lakini hakuwahi
kuwaonesha watanzania mwili wake kama baadhi ya wasanii wanavyofanya,
kwani kitendo hicho endapo angeamua kukifanya basi wazazi wake
wangemchukulia kama limbukemi wa maisha ya mjini.
Kauli
ya msanii huyo inakuja ili kujisafisha kwani wadau wengi wa tasnia ya
filamu kwa sasa hawana hamu nayo, kutokana na vitendo vingi
vinavyofanywa na wasanii wake, ambapo vingine vimekuwa vikiwahawaribu
hata watoto wadogo ambao hupenda sana kutazama kazi zao.