Rais
Baraka Obama akicheza ngoma alipokua akipita kwenye moja ya vikundi
vya ngoma za asili vilivyokua vikitumbuiza kwa ajli ya ujio wake mara
tu aliposhuka kutoka kwenye ndege ya Airforce One
Mwenyeji
wake Rais Jakaya Kikwete akitabasamu wakati mgeni wake Rais Barack
Obama alipokua akitikisa mwili kwa hisia za ngoma za asili zilizokua
zikitumbuizwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa
ujio wake leo akitokea Afrika ya Kusini.
Rais Barack Obama akiangalia moja ya vikundi vya ngoma za asili vilivyokua vikitumbuiza uwanjani hapo.
Rais Barack Obama akikagua majeshi ya ulinzi na usalama.
Rais
wa Marekani Barack Obama pamoja mkwewe wakilakiwa na mwenyeji wao Rais
Jakaya Kikwete mara tu walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa
kiamataifa wa Julius Nyerere leo Jumatatu July 1, 2013 kwa ziara ya siku
2., kushoto ni mama Salma Kikwete.
Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama akipokewa kwa Shangwe Ikulu, Dar es salaam na baadaye akaongea na wanahabari..