Afrika
Kusini ni nchi yenye uchumi mkubwa Afrika ambao umevutia Waafrika wengi
kukimbilia huko kwa ajili ya kufanya kazi kama za Udereva, uuzaji
mafuta kwenye vituo vya mafuta pamoja na kazi nyingine mbalimbali.
Taarifa kutoka kwenye mji wa Pretoria ni kwamba Watanzania ambao
wanamiliki na kufanya biashara mbalimbali zikiwemo za Maduka na wale
wanaomiliki hoteli, wamevamiwa wakiwa kwenye mali zao na kufanyiwa
uharibifu na nyingine kuchomwa moto.
Ni kundi la watu ambalo linaendeleza uvamizi huu ambapo linawashutumu
Watanzania hawa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, yani kwa ufupi
Watanzania wanasema hata kama kweli wangekua wanafanya hii biashara,
walio na mamlaka ya kuwavamia ni Polisi na sio hao raia.
Inaaminika
kundi hili lina sehemu kubwa ya madereva Taxi wazawa wa nchi hiyo ambao
wamekua wakiumizwa na jitihada za raia wa kigeni wa Nigeria na
Watanzania ambao wamejazana kwenye mtaa wao wakimiliki maduka mbalimbali
yakiwemo ya nguo pamoja na hoteli.
Tayari balozi wa Tanzania amekutana na Watanzania hao na kuahidi
kulifatilia ambapo ni Watanzania watano wamejeruhiwa wakiwemo watatu
ambao bado wako hospitali na mmoja wao kavunjika mkono, mmoja kapigwa
kichwani.
Kabla ya Watanzania wengine kuwahi kufunga maduka yao, maduka matatu
ya Watanzania pamoja na hoteli mbili zinazomilikiwa na Watanzania
zilivamiwa na wakachuchukuliwa simu na watu kupigwa ambapo polisi
walipokuja hakuna chochote kilichofanyika zaidi ya maelezo.
Picha hizi zote zilipigwa na Mtanzania akiwa anakimbia baada ya kufanikiwa kufunga duka lake.
Top-ads
HABARI MOTO MOTO
Followers
Popular Posts
-
Zaidi ya watu 300 bado hawajapatikana baada ya meli kubwa iliyobeba watu 459 kuzama huko South Korea ambapo sehemu kubwa ya watu waliokuwe...
-
Rihanna ameingia matatani na mtandao wa Instagram baada ya kuweka picha hizi za uchi, alizopigwa kupamba gazeti la Lui. Mtandao huo ulii...
-
any word about the look ya huyu mrembo ?
-
PADRI AFUMANIWA LIVE NA MKE WA MTU AKIWA UCHI WA MNYAMA KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri w...
-
Stori: Erick Evarist MAAJABU! Licha ya ulimwengu wa burudani Bongo kuamini kwamba staa wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ aliwahi kua...
-
Jarida la People limemtangaza Mkenya Lupita Nyong’o kama mwanamuke mrembo zaidi duniani mwaka 2014. Lupita ambaye alishin...
-
WANA UDOM CHAMBER WATOA ZAWADI YA PASAKA KWA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA MIYUJI KILICHOPO MJINI DODOMA JANA Hii ni moja ya Pic...
-
Morning Africa,...SIKU YA LEO UPATAPO NAFASI,HEBU JARIBU KUFANYA MOJA YA HAYA NA UTAKUWA UMEBADILISHA MAISHA YA MTU FLANI. -Una mlinzi?...
-
FID Q ROCKS VODACOM WAJANJA MUSIC TOUR IN MTWARA Hundreds of Wajanja Music Tour fans in Mtwara were thrilled on Sunday evening by ...
-
HABARI zilizonaswa na mwandishi wetu zinaeleza kuwa nyota wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ameitwa katika Jiji la Dubai...


