Rumours: Selena Gomez ampiga chini Justin Bieber kisa Rihanna!
Mtandao wa MediaTakeOut umeripoti kuwa zipo fununu
mtaani kwamba Justin Bieber na mpenzi
wake wa siku nyingi Selena Gomez wameachana.
Mtandao huo umesema kwa mujibu wa story za mtaa ni kwamba Selena
Gomez amempiga chini Justin, baada ya kusikia fununu kuwa Justin na Rihanna wamekuwa
karibu sana, na Selena anahisi huenda wameshavunja amri ya sita.
Na fununu za ukaribu huo wa Rihanna-Beiber umemkera pia CHRIS
BROWN kiasi cha kumfanya amtukane kwenye remix yake ya Theraflu.
Mtandao huo umeendelea kuyaunganisha matukio yanayosupport
fununu hizo kwa kudai kuwa Justin alihudhuria tuzo za BILLBOARD siku mbili
zilizopita akiwa peke yake bila Selena kitu ambacho si kawaida.
Ushahidi mwingine ni kuwa
Selena ameacha kumfollow Justin kwenye Twitter!!!