WEMA NA AUNT EZEKIEL WAPEWA BARUA
Kitendo kilichofanywa na wasanii wawili wanaotamba katika soko la filamu
nchini Wema Sepetu na Aunt Ezekiel kupanda jukwaani huku wakionesha
sehemu kubwa ya maungo yao ya mwili vimeonekana kuwakera wadau
mbalimbali wa tasnia ya sanaa nchini
Akizungumza na mwandishi wa habari hii mwenyekiti wa Chama cha Watunzi
wa Miswaada ya Filamu Tanzania (TASA) Abdul Lihinda alisema kitendo hiko
kinadharilisha soko la filamu Tanzania na tasnia nzima ya filamu
Alisema kama msanii ni kioo cha jamii na wanajamii wanategemea mambo
mengi mazuri kutoka kwako hivyo kinachofanyika ni kudharirisha tasnia
hiyo
Aliongezea kuwa kitendo hiko kimewakasilisha pia hata Shirikisho la
Filamu Tanzania (TAFF) na teyari hatu za awali zimeshachukuliwa kwa
kuwaandikia barua wasanii hao wawili ambayo barua nyingine imepelekwa
wizara ya Habari Utamaduni na Michezo na hatua nyingine zinaendelea
kufuatwa ili kukomesha uchafu huo.
CHANZO PRO24

