kutana na msanii wa Komedi na Bongo Fleva, Musa Yusuph
‘Kitale’. Hapa amefunguka juu ya uhusiano wake na marehemu Ramadhan
Mkiety ‘Sharo Milionea’ aliyefariki dunia Novemba, mwaka jana.
Funguka: Mambo vipi Kitale, shemeji yetu hajambo?
Kitale: (Kicheko kidogo) Hajambo, mzima wa afya, vipi!
Funguka:
Moja kwa moja tuanzie kwenye uhusiano wako na marehemu Sharo Milionea,
tunatambua alikuwa swahiba wako mkubwa, staili yenu ya maisha ilikuwaje?
Kitale:
Kiukweli pengo la marehemu kwangu litabaki palepale. Tukiachilia mbali
ushirikiano wetu kwenye kazi, alikuwa rafiki yangu mkubwa ndani na nje
ya gemu. Tulisaidiana kwa mambo mengi sana, sidhani kama nitapata rafiki
mwingine kama yeye.
Funguka: Pole sana, mbali na huo ukaribu kuna kitu gani ambacho unakikumbuka na pengine kinakurudiarudia akilini mwako?
Kitale:
(Akaongea kwa huzuni) Dah! tulikuwa na mipango mingi sana kuhusu muziki
na maigizo tuliyokuwa tunayafanya, kubwa zaidi tulipanga kuoa kwa
pamoja. ‘So’ nilivyopata habari za kifo chake, mipango yote iliharibika
hadi nilipokuja kujipanga upya. Tukio hilo hujirudia sana akilini
mwangu.
Funguka: ‘Anyway’, ndoa yako ilikuwa wazi na kila mtu anamjua
shemeji, unaweza kututajia hata jina la huyo aliyekuwa mtarajiwa wa
marehemu?
Kitale: Mh! Hapana labda siku mwenyewe akiniruhusu kumtaja nitafanya hivyo.
Funguka: Watu wanasema wewe ndiye mrithi wa Sharo Milionea, unazungumziaje ishu hiyo?
Kitale:
Dah! Nilikuwa sijui, ila mimi sioni tatizo ingawa kwa upande wangu
naona kama tulikuwa na ladha tofauti, japo tuna wasifu unaofanana.
Funguka: Kitale tunashukuru kwa ushirikiano wako, kazi njema.
Kitale: Nashukuru, tuchekiane ‘next time’.
Top-ads
HABARI MOTO MOTO
Followers
Popular Posts
-
Zaidi ya watu 300 bado hawajapatikana baada ya meli kubwa iliyobeba watu 459 kuzama huko South Korea ambapo sehemu kubwa ya watu waliokuwe...
-
Rihanna ameingia matatani na mtandao wa Instagram baada ya kuweka picha hizi za uchi, alizopigwa kupamba gazeti la Lui. Mtandao huo ulii...
-
any word about the look ya huyu mrembo ?
-
PADRI AFUMANIWA LIVE NA MKE WA MTU AKIWA UCHI WA MNYAMA KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri w...
-
Stori: Erick Evarist MAAJABU! Licha ya ulimwengu wa burudani Bongo kuamini kwamba staa wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ aliwahi kua...
-
Jarida la People limemtangaza Mkenya Lupita Nyong’o kama mwanamuke mrembo zaidi duniani mwaka 2014. Lupita ambaye alishin...
-
WANA UDOM CHAMBER WATOA ZAWADI YA PASAKA KWA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA MIYUJI KILICHOPO MJINI DODOMA JANA Hii ni moja ya Pic...
-
Morning Africa,...SIKU YA LEO UPATAPO NAFASI,HEBU JARIBU KUFANYA MOJA YA HAYA NA UTAKUWA UMEBADILISHA MAISHA YA MTU FLANI. -Una mlinzi?...
-
FID Q ROCKS VODACOM WAJANJA MUSIC TOUR IN MTWARA Hundreds of Wajanja Music Tour fans in Mtwara were thrilled on Sunday evening by ...
-
HABARI zilizonaswa na mwandishi wetu zinaeleza kuwa nyota wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ameitwa katika Jiji la Dubai...


