NIMENYOWAAA JAMANI...HAPOO VIP
By Alberto | 4:08 AM
WEMA Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ ametengeneza kichwa cha habari kingine, safari hii amekuja na muonekano mpya, amenyoa nywele.
Kama kawaida yake huwa hakosei, Jumatano wiki hii kupitia mtandao wa Instagram, Beautiful Onyinye alitupia picha inayomuonesha akiwa katika muonekano huo mpya.
Kupitia mtandao huo, maoni kibao yalimiminika kupongeza muonekano mpya wa mwanadafada huyo asiyekaukiwa matukio Bongo.
Paparazi wetu alipojaribu kumdodosa kulikoni mlimbwende huyo afikie uamuzi wa kunyoa nywele na kuachana na muonekano wa zamani, Wema alisema ameamua kubadilika kidogo kwani siku zote hapendi watu wamzoee katika muonekano uleule.