KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji na kata ya Mkwajuni
Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wamemzika Mwanakijiji mwenzao akiwa hai
wakimtuhumu kusababisha kifo cha Mkazi mmoja kijijini hapo.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Apri 26 mwaka huu majira ya Saa Nane
Mchana katika Kitongoji cha Maweni Makaburini baada ya Mhanga
aliyefahamika kwa jina la Victory Mwachirui(68) kuhudhuria mazishi ya
Pita Barton(28)aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Thobias Ismail amesema marehemu
alipatwa na mauti akiwa anapatiwa matibabu kwa mganga wa jadi ambaye
jina lake halikuweza kujulikana maramoja.
Amesema wakati taratibu za mazishi zikiendelea Ndugu wa marehemu walidai
kuwa kifo cha Marehemu kilisababishwa na Mwachirui ambaye ni Katekista
mstaafu kwa imani za kishirikina.
Ameongeza kuwa wakati kaburi likichimbwa kwa ajili ya kumzika marehemu
ndipo vijana waliokuwa wakichimba waliagiza Wazee wa Mila wafike
makaburini kwa ajili ya kuangalia utaratibu wa mazishi na kukagua ukubwa
wa Kaburi ambalo lilikuwa limekwisha chimbwa.
Kutokana na mwito huo walifika wazee wanne akiwemo Mzee Mwachirui ambaye
walimsisitiza kusogea jirani na kaburi ambapo baada ya kusogea alipigwa
na Sururu kichwani na kuangukia kaburini huku akisindikizwa na
marungu..

Jeneza la aliyekufa kwa ugonjwa tayari limetolewa pembeni. Sasa anafukuliwa aliyezikwa akiwa hai

Mwili wa aliyezikwa hai unatolewa kaburini

Dada wa marehemu aliyezikwa akiwa hai