Sitti Abas Mtemvu amevuliwa taji la Miss Tanzania 2014 baada ya kuiandikia kampuni inayohusika na mashindano hayo, Lino International Agency kutoa uamuzi wake rasmi wa kujivua taji hilo.
Akielezea uamuzi huo, unaotokana na shutuma za kudanganya umri, mrembo huyo ameandika
Baada ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania kumezuka shutuma mbalimbali dhidi yangu. Wameniwekea maneno mengi sana mdomoni kwamba nimesema wakati siyoBaada ya uamuzi huyo, aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Deus Kamanzima amerithi taji hilo. Zifuatazo ni picha za Miss Tanzania huyo mpya
Shutuma hizo zimeandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari, blogs na mitandao ya kijamii, kiasi ambacho naweza hata kuhatarisha maisha yangu. Sasa kwa hiari yangu tena bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima yangu na familia yangu natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania 2014.
Napenda niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa. Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu.
Leo nalivuta taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo niliochukua.