Picha aliyopost Instagram Waziri wa Vijana na Utamaduni (Youth and Culture Minister) wa Jamaica, Lisa Hanna, imezua gumzo na malalamiko. Baadhi ya wananchi wa Jamaica wamefunguka
katika mitandao ya kujamii wakisema kuwa ni kinyume cha maadili na
udhalilishaji wa nchi yake kwa waziri kupost picha akiwa nusu-uchi.
Picha hiyo inayodaiwa kupigwa na mwanae Alexander Panton baada ya Reggae Marathon, inamuonyesha mwanasiasa huyo akiwa beach, amevaa yellow two-piece bikini na fulana yenye picha ya marehemu Bob Marley

Picha
aliyopost Waziri wa Vijana na Utamaduni wa Jamaica akiwa ndani ya
bikini, iliyozua gumzo na kulaaniwa na baadhi ya wananchi wa nchi hiyo
Lakini kwa msiomjua, waziri Lisa Hanna si mwanasiasa wa kawaida, kwani alikuwa Miss Jamaica, na alitwaa taji la Miss World 1993. Enzi zake alikuwa ni mmoja wa warembo wakali kuliko duniani, na hata sasa ni bado mkali.
Hii
si mara ya kwanza kwa waziri Hanna kupost picha ya swimsuit. Miezi
mitano iliyopita alipost picha hii; lakini tofauti ni picha hii aliipiga
miaka 10 iliyopita, kabla ya kuingia kwenye siasa
Baadhi ya Wajamaica, akiwemo Senator wa kike Marlene Malahoo Forte, wamemtetea waziri huyo wakisema kivazi alichovaa ni muafaka kwa beach. Waziri Lisa Hanna mwenyewe hajatoa kauli yoyote kuhusu ishu hiyo na anaendelea kupost picha Instagram na raha zake. Vipi unaonaje? Amechemsha au ni sahihi?

Akiwa saloon akisubiri kutengenezwa nywele, huku akikuonyesha kinyemela kuwa usafiri bado wamo

Ni mmoja wa wanasiasa wakali katika “high-fashion.” Of course alishawahi kuwa Miss World, hivyo lazima a-represent